![]() |
Mkaguzi wa Fifa Domenico Scala |
Afisa wa ukaguzi katika shirikisho
la soka duniani Fifa Domenico Scala,amejiuzulu akipinga mabadiliko
yanayofanyika katika shirikisho hilo.
Baraza hilo lilichukua mahala pa kamati kuu ya Fifa kufuatia madai ya ufisadi katika shirikisho hilo.
''Kamati hizo sasa zitakuwa hazina uhuru kutekeleza majukumu yake'',alisema Scala.
Ameongezea kuwa: Hatua hiyo inahujumu nguzo ya uongozi mzuri wa Fifa na inaharibu ufanisi wa mabadiliko yaliofanywa.
Scala alikuwa na jukumu muhimu katika kusukuma mabadiliko kufuatia kashfa iliolazimu kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter na mwenzake wa Uefa Michel Platini.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten