![]() |
Papa Francis akikutana na kiongozi mkuu wa chuo kikuu cha kiislamu nchni Misri Al-Azhar |
Kiongozi mmoja wa kidini nchini
Misri amefanya mazungumzo na Papa Francis ,ikiwa ni ishara za hivi
karibuni za kutaka kuimarisha uhusiano kati ya dini hizi mbili kubwa
duniani.
Mkutano huo unajiri miaka mitano baada ya Al-Azhar kusitisha mazungumzo na Vatican kufuatia tofauti kubwa na aliyekuwa Papa Benedict wa kumi na sita.
Mwaka 2006,Papa Benedict aliwashangaza Waislamu alipomnukuu kiongozi mmoja wa Byzantine akisema kuwa baadhi ya mafunzo ya mtume Muhammad yalikuwa ya ''kishetani na yasio na utu'',madai ambayo Waislamu wanakana.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten