Lionel Messi
Lionel Andrés Messi (amezaliwa Rosario, Argentina, 24
Juni 1987) ni mchezaji wa mpira
wa miguu kutoka nchi ya Argentina.
Maisha
Alizaliwa akiwa njiti
(yaani kabla ya miezi 9), akachukuliwa na Barcelona akiwa na umri wa miaka
nane (8). Akalelewa ndani klabu ya kukuzia vipaji ya
Barcelona inayofahamika kama Katalunya (Catalan), akichezea timu ya watoto akiwa ndiye mwenye umri mdogo zaidi.
Alianza kuchezea timu ya
wakubwa mwaka 2003, akiwa anavaa namba 19 mgongoni,wakati namba 10 ilikuwa
inavaliwa na Mbrazili Ronaldinho.
Aliaanza kuingia kwenye historia ya soka duniani mwaka 2009 baada ya kuiwezesha
Barcelona kutwaa ubingwa wa klabu bingwa Ulaya (UEFA), na FIFA kumpa tuzo ya mwanasoka bora wa
dunia.
Aliendeleza historia na
kuweka historia ya pekee duniani kwa kuchukua tuzo hiyo mara 4 mfululizo.
Sifa za Lionel Messi baada ya kushindia taji la Ballon D'or
Hatua ya Lionel Messi
kunyakua taji la mchezaji bora katika mchezo wa soka duniani kwa mara ya tano
na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufikia kiwango hicho,
inaweka wazi mafanikio ya mshambuliaji huyu matata.
Messi mwenye umri wa miaka
28 raia wa Argentina, alianza kuichezea Barcelona mwaka 2001 akiwa kijana
chipukizi na hadi sasa bado anakipiga na klabu hiyo.
Kuendelea kuichezea
Barcelona kumemjenga na kumfanya kuwa na nidhamu nje ya ndani ya uwanja.
Unyenyekevu wa Messi pia
umemsaidia katika uchezaji wake na hata alipotangazwa mshindi alionekana
mtulivu na hata kuwapa mkono wenzake, Neyma na Christiano RonaldoMessi
amekuwa mfungaji bora
katika ligi kuu nchini Uhispania La Liga mara 3, msimu wa mwaka 2009-2010
alifunga mabao 34, 2011-2012 akafunga mabao 50 na msimu wa mwaka 2012-2013
alifunga mabao 46.
Amewahi pia kuongoza katika
ufungaji wa mabao katika michuano ya klabu bingwa mara tano, mwaka 2008-2009
alifunga mabao 9, 2009-210 mabao 8, 2010-2011 mabao 12, mwaka 2011-2012 mabao
14 na mwaka 2014-2015 mabao 10.
Messi ameisaidia klabu yake
kushinda mataji yafuatayo:
·
Klabu bingwa barani Ulaya mara 4 : 2005-06, 2008-09, 2010-11,
2014-15
·
Kombe la dunia kwa vlabu (3): 2009, 2011, 2015
·
Taji la Super Cup barani Ulaya (3): 2009, 2011, 2015
·
Ligi kuu ya soka nchini Uhispania (7): 2004-05, 2005-06,
2008-09, 2009-10, 2010-11, 2012-13, 2014-15
Rekodi zake mpya hizi hapa Lionel Messi amefunga magoli 15
katika mechi 13 za UEFA Ligi ya Mabingwa dhidi ya timu za Uingereza.
Goli la kwanza la kwenye mchezo huo lilikuwa ni goli la 100 kwa
safu ya MSN kwenye mashindano yote kwa mwaka 2016.
Messi kwa sasa anaongoza orodha ya wafungaji katika viwanja vya
nyumbani kwenye michuano ya Ulaya akiwa mefunga magoli 50
Geen opmerkingen:
Een reactie posten