![]() |
| Waziri wa michezo Fikile Mbalula |
Afrika Kusini haitaandaa mashindano
ya Raga, Kriketi, Riadha na Netiboli baada ya serikali kupiga marufuku
shirikisho hizo nne kwa kukikuka kanuni zinazopendekeza kuwepo kwa
wachezaji weusi katika timu za taifa.
Waziri Mbalula alisema kuwa serikali haitaruhusu kamwe uwenyeji wa mashindano hayo manne kwa sababu yameshindwa ketekeleza matakwa yao kikatiba kuongeza idadi ya wachezaji weusi katika timu za taifa.
Kauli hiyo ni pigo kubwa kwa shirikisho la raga la Afrika Kusini kwani ilikuwa imepanga kuwania uwenyeji wa mashindano ya dunia ya mwaka wa 2023.
![]() |
| Afrika Kusini yapiga marufuku michezo minne |
Aidha Mbalula amekuwa akiishawishi shirikisho hilo la raga kuwakuza wachezaji weusi bila mafanikio.
Mashirikisho hayo makubwa ya michezo nchini humo yalitia sahihi mkataba wa kuimarisha idadi ya wachezaji weusi mwaka wa 2014 hata hivyo kufikia sasa ni shirikisho la kandanda pekee lililotimiza matakwa hayo.
Hii inamaanisha kuwa mashirikisho hayo manne hayataruhusiwa kuandaa ama hata kuwania uwenyeji wa mashindano yeyote ya kimataifa.
Kamati maalum itakutana mwishoni mwa mwaka wa 2018 kutathmini maendelea ya mashirikisho hayo manne.
Marufuku hiyo hata hivyo haitaathiri uwenyeji wa michezo ya jumuiya ya madola ya mwaka wa 2022 ambayo imeratibiwa kufanyika mjini Durban Afrika Kusini.




Geen opmerkingen:
Een reactie posten