Rais wa Rwanda Paul Kagame amekana
madai yaliotolewa na Umoja wa Mataifa kwamba taifa lake linaendelea
kuwasaidia waasi katika nchi jirani ya Burundi.
Burundi imekabiliwa na mgogoro mbaya wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kupigania muhula mwengine mwaka uliopita.
Ni mwaka mmoja kamili tangu rais Nkurunziza kuepekua jaribio la mapinduzi.
Rwanda ilikana madai kama hayo kuhusu kuwaunga mkono waasi katika ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Februari.
Bw Kagame amekosoa wachapishaji wa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baadaye,ikisema mda wake ungetumika vyema kuangazia matatizo yanayokumba mataifa badala ya kuyazidisha.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten