![]() |
Ndege moja ya shirika la ndege la
Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi
Cairo, imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya Misri.
Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga.
Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki
Geen opmerkingen:
Een reactie posten