Wanaharakati nchini Nigeria wanasema
kuwa mmoja wa wasichana wa shule wa Chibok, waliotekwa nyara na kundi
la Boko Haram amepatikana, akiwa ndiye mtu wa kwanza kukolewa kwa zaidi
ya miaka miwili.
Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na
wanamgambo wa Boko Haram kutoka mji ulio Kaskazini Mashariki mwa Nigeria
zaidi ya miaka miwili iliyopita. Mwanaharakati Hauwa Abdu aliiambia BBC kuwa,
msichana huyo alipatikana siku ya Jumanne jioni na kundi moja la kuweka
ulinzi baada ya makabiliano na watu wanaokisiwa kuwa wapiganaji wa Boko
Haram.
Kiongozi mmoja wa kijamii alisema kuwa msichana huyo
alikuwa na mtoto na wote wamekabidhiwa jeshi la Nigeria katika mji wa
Damboa.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten