Kundi la watu wanaojidai kuwa
wapiganaji wa Kiislamu limeweka video mtandaoni likidai uwepo wa wa
wapiganaji wa Kiislamu nchini humo.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga na kampeni yao.
Ukurasa wa Twitter ambao unasambaza video hiyo ya dakika tano unasema wanaume hao ni tawi la Afrika Mashariki la kundi linalojiita Islamic State (IS).
Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya usalama Afrika, Tomi Oladipo, anasema hakuna ushahidi wa uhusiano wa moja kwa moja kati ya wapiganaji hao na kundi la Islamic State
Geen opmerkingen:
Een reactie posten