Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola
anasema kuwa amekuwa kocha bora zaidi katika misimu yake mitatu katika
klabu hiyo wakati ambapo anajiandaa kucheza mechi yake ya mwisho katika
ligi hiyo.
''Nimejifunza mengi kutoka kwa wachezaji wangu.Ninafurahia uamuzi wangu wa kuja hapa''.
Mechi yake ya mwisho itakuwa mechi ya kombe la Ujerumani kati ya timu yake na Borussia Dortmund Jumamosi ijayo huku akitarajia kushinda kombe la pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten