burudan

HII NDO ILIKUWA VITA YA CAROLL DHIDI YA ARSENAL

Andy Caroll alifunga mabao matatu na kuiwezesha West Ham kuizuia Arsenal na hivyobasi kuvunja matumaini ya timu hiyo kushinda taji la ligi ya Uingereza.

Arsenal sasa iko pointi 10 nyuma ya Leicester ikiwa imesalia mechi sita.

Mesut Ozil na Alexis Sanchez waliiweka Arsenal kifua mbele kufuatia pasi nzuri za Iwobi ,lakini Caroll alifunga mabao mawili ya ghafla ndani ya sekunde 160 ili kusawazisha.

Kichwa kizuri katika kipindi cha pili kilimpatia Andy Caroll bao lake la tatu ,kabla ya beki wa Arsenal Laurent Koscielny kusawazisha.

Hatahivyo West Ham iliongeza rekodi yake ya kutofungwa katika ligi ya Uingereza na kufikia mechi 14 wakiwa nyumbani ,lakini kikosi hicho cha kocha Slaven Bilic kinasalia nafasi ya sita katika jedwali la ligi ya Uingereza.

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates