![]() |
Ndege hiyo iliwauwa abiri wote 66 waliokuwemo. |
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi,
anasema kuwa kila kitu kinachoaminiwa kusababisa ajali, kinasalia jinsi
kilivyo kuhusiana na ajali ya ndege ya EgyptAir, iliyoanguka siku ya
Alhamisi.
Hapo jana Jumamosi, wachunguzi wa Misri walisema ni mapema mno kufikia hatma ya kilichosababisha ajali hiyo kwani uchunguzi wa data bado haujakamilika.
Kikosi kinachoendelea na msako kinaendelea kutafuta mabaki ya ndege hiyo pamoja na kisanduku cha kuhifadhi mawasiliano ya ndege.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten