burudan

Ndege zashambulia barabara karibu na Allepo, Syria

Ndege zilifanya mashambulizi kwenye barabara inayoelekea maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Allepo.
Wanaharakati nchini Syria wanasema kuwa ndege za kivita zimefanya mashambulizi makubwa zaidi kwenye barabara inayoelekea maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Allepo.

Wanaharakati wanasema kuwa ndege za Urusi na za serikaliya Syria, zimeshirika kwenye mashambulizi hayo licha ya hilo kutothibitishwa rasmi.

Serikali ya Syria imekuwa ikishambulia maeneo yanayodhibitiwa na waasi mjini Allepo siku za hivi karibuni na kuvunja makubaliano yaliyoafikiwa mwishoni mwa mwezi Februari.

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates