Wavamizi wa kujitolea muhanga
walioishambulia mji mkuu wa Ubelgiji , Brussels mwezi uliopita walikuwa
wanalenga kuishambulia upya Ufaransa.
Afisi ya kiongozi wa mashtaka mjini Brussels tayari wameshafichua uhusiano baina ya washambuliaji hao wa Brussles na wale waliotekeleza mashambulizi mjini Paris Ufaransa mwezi Novemba mwaka uliopita.
Shambulizi lilisababisha vifo vya watu 130.
Aidha wamethibitisha kumfungulia mashtaka mshukiwa mkuu wa mashambulizi hayo bwana Mohammed Abrini, ambaye alihusika katika shambulizi la Brussels na vilevile lile la Paris.
Mshukiwa huyo alinaswa na kamera fiche akiwa na walipuaji wa kujitolea muhanga lakini akatoweka baada ya ukanda wake uliojaa vilipuzi kukosa kulipuka.
Viongozi wa mashtaka walisema kuwa Mohamed Abrini alikiri kuwa yeye ndiye aliyekuwa mtu wa tatu aliyeonekana kwenye picha za CCTV akisukuma troli
Yeye ni mmoja wa watu wanne walioshtakiwa na polisi wa Ubelgiji hiyo jana kwa kushiriki katika milipuko iliyotokea kwenye uwanja wa ndege na njia ya chini kwa chini ya treni.
Yeye pia ameshirikishwa na mashambulizi ya Paris ya Novemba mwaka uliopita yaliyosababisha vifo vya watu 130.
Mwingine aliyeshtakiwa ni raia wa Sweden Osama Krayen, ambaye ametambuliwa kama mtu aliyeonekana akuzungumza na mshambulizi wa kujitoa mhanga katika mtandao wa treni wa Malbeek muda mfupi kabla ya shambulio.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten