Ndege za kijeshi nchini Nigeria zimeshambulia ngome muhimu ya
kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram na kulitia hasara kubwa.
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, jana kikosi cha anga nchini humo, kilitekeleza shambulio hilo kwenye ngome ya kilojestiki ya Boko Haram katika eneo la Kangaroo lililopo katika jimbo lenye machafuko la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, miripuko kadhaa na moto mkubwa vilishuhudiwa katika eneo hilo na hivyo kulifanya jeshi hilo kujawa na imani kwamba, ngome hiyo ilikuwa mahala muhimu pa kuhifadhia silaha kwa ajili ya genge hilo la Boko Haram.
Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imetangaza kuwa, katika miezi iliyopita, kundi hilo la kigaidi lilipata kipigo kikali kutoka kwa majeshi ya nchi za eneo la magharibi mwa Afrika. Hata hivyo jeshi hilo la Nigeria limeonyesha masikitiko yake juu ya kuendelea vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na wanachama wa Boko Haram huku likisisitiza juu ya udharura wa kutokomezwa
Geen opmerkingen:
Een reactie posten