Watu 46 wameripotiwa kuuawa ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya
mwanzoni mwa mwaka huu katika ghasia zinazoendelea nchini Burundi.
Wizara ya Usalama wa Uma nchini Burundi imetangaza kuendelea
machafuko ambapo watu 46 wameuawa tokea mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016
pekee. Kwa mujibu wa wizara hiyo katika machafuko hayo, watu wengine 215
wamejeruhiwa.
Hata hivyo Alain-Guillaume Bunyoni Waziri wa Usalama wa Uma nchini humo ameongeza kuwa, hali ya mambo imeboreka kidogo mwezi huu wa April ikilinganiswa na miezi iliyopita.
Amewatuhumu wapinzani wa serikali kuwa waroho wa madaraka na kuwahusisha na machafuko hayo ye
nye lengo la kuharibu usalama wa taifa hilo.
Mwaka mmoja umetimia tangu Burundi itumbukie katika hali ya mchafukoge mwezi Aprili mwaka jana, kufuatia hatua ya chama tawala cha CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza kugombea tena urais katika uchaguzi uliopita nchini humo.

Geen opmerkingen:
Een reactie posten