Wanasayansi nchini Brazil wamezema
kuwa virusi vya ZIKA ambavyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wakiwa
na vichwa vidogo huenda ni hatari zaidi kuliko ilivyofikiriwa awali.
Madaktari wengi na watafiti sasa wanakubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye ubongo.
Lakini wakati asilimia moja ya wanawake walioathiriwa na virusi vya Zika wakati wa ujauzito kuelezwa kuwa watapata watoto wenye vichwa vidogo, Madaktari nchini Brazil wameiambia BBC kuwa asilimia ishirini ya mimba zilizoathiriwa na ZIKA zitasababisha aina nyingine ya kuharibiwa kwa ubongo wa mtoto akiwa tumboni.
Kasi ya maambukizi katika baadhi ya sehemu nchini Brazil imepungua kutokana na elimu iliyotolewa kuzuia maradhi hayo, hata hivyo hati hati za kusaka chanjo ya kupambana na Virusi bado ziko katika hatua za awali, huku hatari ikiendelea kuwepo katika ukanda wa Amerika ya kusini.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten