Mkurugenzi wa CIA John Brennan
amesema kwa miaka mitano iliyopita Marekani imeharibu kwa kiasi kikubwa
kundi la Al Qaed baada ya kuuawa kwa kiongozi wake mkuu Osama bin Laden
baada ya uvamizi wa vikosi maalum nchini Pakistan.
Bw Brennan
amesema kuwa Bin Laden alikua nembo na mwenye mikakati imara na muhimu
na ilikua lazima kumuondoa mtu huyo ambaye alihusika katika mashambulizi
ya kigaidi mjini Washington na New York Septemba 11. Mkuu huyo wa CIA ameongeza pia kumuondoa kiongozi wa
wa IS Abu Bakr Al-Baghdadi inaweza kuwa na athari kubwa.Lakini
akaongeza kuwa vitendo vya kigaidi vinaathiri dunia nzima na changamoto
hiyo itakua kwa miaka mingi ijayo.
CIA inasherekea miaka mitano
tokea kuuawa kwa Bin Laden kwa kuelezea namna walivyofanikisha kukamatwa
kwake kama jambo lililotokea siku za karibuni.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten