Maelfu ya watu wanatarajiwa
kujitokeza leo mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za rumba
Papa Wemba.
Wemba, 66, aliyesifika kote duniani kama mmoja wa wanamuziki nguli wa nyimbo za rumba kutoka DR Congo, alifariki baada ya kuzirai akitumbuiza mjini Abidjan wiki moja iliyopita.
Alipendwa sana na mashabiki kwa nyimbo zake na pia mtindo wake wa mavazi.
Rais Joseph Kabila ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ya wafu leo kwa heshima ya marehemu mjini Kinshasa.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten