Meli ya kifahari ya Marekani imeanza
safari yake kuelekea Cuba ikitokea nchini Marekani kwa mara ya kwanza
katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
Meli hiyo
iitwayo Adonia, imebeba abiria wapatao mia saba,imeng'oa nanga kutoka
katika bandari ya Miami na inatarajiwa kufika tamati ya safari yake
Jumatatu ijayo.
Cuba na Marekani zimerejesha uhusiano baina yao wa
kidplomasia mwaka wa jana, ingawaje vita baridi iliyokuwa baina ya nchi
hizo ilisababisha hali kibiashara kati yao kuwa ya kusua sua na bado
hali si shwari mpaka sasa. Safari hiyo ya kihostoria kwa njia ya maji imepiga
hatua moja kubwa mbele katika kuuimarisha uhusiano huo wa kidlomasia na
hii ni baada ya serikari ya Cuba kukubali kuondoa marufuku ya raia wake
kuingia nchini Marekani ama kutumia maji kama njia ya usafiri kuingia
nchini humo
Geen opmerkingen:
Een reactie posten