burudan

CIA yashutumiwa mtandaoni kwa sababu ya Osama

Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) limeshutumiwa mtandaoni kwa kusimulia moja kwa moja matukio yaliyopelekea kuuawa kwa Osama Bin Laden.

Shirika hilo limekuwa likiandika ujumbe kwenye Twitter na kusimulia matukio yaliyopelekea kuuawa kwa kiongozi huyo wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda kana kwamba yalikuwa yanafanyika leo.
Siku ya leo ni miaka mitano tangu kuuawa kwa Osama Mei 2011 katika nyumba moja mjini Abbottabad, Pakistan.
Alikuwa amesakwa na Marekani na washirika wake kwa mwongo mmoja.
CIA wamekuwa wakitoa maelezo kuhusu mipango na ukusanyaji wa habari za kijasusi ambazo zilipelekea Osama kuuawa.

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates