Baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu kasi ya kuimarika kwa
ushirikiano kati ya kundi la wapiganaji la Boko Haram nchini Nigeria na
lile la Islamic State, wakati Nigeria inaandaa kongamano la kupambana na
kundi hilo la kigaidi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari,
baraza hilo la wanachama 15 limesema kuwa Boko Haram linaendelea kuwa
tishio kwa amani na usalama wa mataifa ya Afrika Magharibi na Afrika ya
kati. Boko Haram lilitangaza utiifu wake kwa Islamic State
mwaka jana, na inaripoitiwa kuwa liliwatuma wapiganaji wake kuungana na
Islamic State nchini Libya.
Baraza hilo pia limekaribisha
kongamano lililoandaliwa na rais wa Nigeria Mohamadu Buhari siku ya
Jumamosi, kuangazia upya jitihada za kupambana na wapiganaji hao. Kongamano hilo litahudhuriwa na viongozi wa kikanda pamoja na rais wa ufaransa Francois Hollande.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten