
Ibrahimovic anahusishwa na kujiunga na Manchester United, Los Angeles Galaxy na AC Milan ingawa hamna habari rasmi mbali ya kuthibitika hii Leo kuagana na PSG ambayo amekuwa nayo kwa Miaka Minne.
PSG, ikithibitisha kupeana mkono na Ibrahimovic, imetamka kuwa Straika huyo ni mahiri mno na ni mmoja wa Wachezaji Bora katika Historia ya Klabu yao.
Kwa mujibu wa Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, Staa huyo huenda akarea tena Klabu hapo kwa vile yapo makubaliano ya jambo hilo.
Mwenyewe Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, ametamka: “Nilikuja kama Mfalme, naondoka Lejendari ila nitarudi!”
Licha ya kujiunga na PSG Mwaka 2012, Ibrahimovic ameweka Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa PSG katika Historia yao akiwa na Bao 152 katika Mechi 178.
Tangu wakati huo, kila Msimu PSG imetwaa Ubingwa wa France na Msimu huu wametetea Taji lao huku kukibaki Miezi Miwili Ligi kumalizika.
Pia Ibrahimovic amekuwa Mfungaji Bora wa Ligi 1 katika Misimu ya 2012-13 na 2013-14 na Msimu huu anaongoza akiwa Bao 15 mbele ya wa Pili Alexandre Lacazette wa Lyon.
Jumamosi, PSG watakuwa kwao kufunga Msimu wa Ligi 1 kwa kucheza na Nantes na kisha kukutana na Marseille katika Fainali ya Kombe la France hapo Mei 21 kufunga rasmi Msimu wa Soka.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten