burudan

Jay Z kufanya album atakayofunguka kuhusu tetesi za usaliti kama jibu kwa Beyonce na album yake yaLemonade

Mtu wa karibu na familia ya The Carter ameliambia jarida la US Weekly kuwa rapa Jay Z anarekodi nyimbo zitakazoeleza upande wake wa kilichotokea kwenye ndoa yake na rnb staa Beyonce.
Queen Bey  aliwashangaza mashabiki kwa video maalum iliyorushwa na HBO pamoja na album ya Lemonade. Video hii ilielezea tetesi za muda mrefu za usaliti wa mume wake kwa mashairi kama ya ” This is your final warning / You know I give you life / If you try this s‑‑t again / You gon’ lose your wife”.
Uvumi wa miaka miwili nyuma ulisema Jay Z na B walikuwa mbioni kuachana kabisa baada ya tukio la ugomvi kwenye lifti. May 2014, TMZ walivujisha video inayomuonesha mdogo wake Beyoncé, Solange Knowles, akimshambulia Jay Z wakiwa kwenye lifti baada ya kuhudhuria hafla ya Met Gala.

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates