![]() |
Cruz na Kasich wanataka kumzuia Trump kushinda majimbo zaidi |
Wapinzani wawili wakuu wa Donald
Trump katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea urais wa chama cha
Republican nchini Marekani wametangaza mipango ya kuungana kukabiliana
na mgombea huyo.
Cruz, ambaye ni seneta wa jimbo la Texas, amesema atapunguza kampeni zake katika majimbo ya Oregon na New Mexico.
Kwa upande wake John Kasich, ambaye ni gavana wa Ohio, naye amesema atamwachia Cruz katika mchujo ujao jimbo la Indiana.
Bw Trump ameshinda majimbo mengi kufikia sasa, lakini bado hajapata wajumbe wanaohitajika kumpa ushindi wa moja kwa moja kabla ya Kongamano Kuu la Kitaifa la Chama mwezi Julai.
![]() |
Bw Trump amekuwa akisema viongozi wa chama hawataki ashinde |
Wapinzani wake wanasema iwapo Trump ataidhinishwa kuwa mgombea wa Republican basi chama hicho hakitaweza kushinda uchaguzi mkuu mwezi Novemba dhidi ya chama cha Democratic.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten