![]() |
Wanajeshi hao hata hivyo hawatashiriki moja kwa moja katika vita |
Maafisa wakuu nchini Marekani
wanasema kuwa Rais Barack Obama atatuma wanajeshi ya ziada wapatao 250
nchini Syria, ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani
vya nchi hiyo, katika kupambana na wapiganaji wa Islamic State.
Hata hivyo vikosi hivyo vya Marekani havitawajibika moja kwa moja katika mapambano hayo.
2. Jopo lasema serikali Mexico ilitatiza uchunguzi
![]() |
Wanafunzi 43 walitoweka mwaka 2014 |
Wataalamu hao wanapuuzilia mbali taarifa ya mwisho kwamba waalimu hao walipeanwa kwa genge la majambazi na maafisa wafisadi wa polisi.
Inasemekana kuwa genge hilo liliteketeza miili ya wanafunzi hao katika eneo la utupaji taka.
3. Mvulana wa miaka 16 ashtakiwa ugaidi Australia
Mvulana huyo alitiwa mbaroni nyumbani kwake huko Sydney, alipodaiwa kupanga kutekeleza uhalifu huo wa kigaidi leo Jumatatu wakati wa sherehe za siku kuu ya ANZAC, ya maadhimisho hayo ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa vitani Australia.
4. Chama tawala chashinda uchaguzi Serbia
![]() |
Ushindi huo unachukuliwa kama uungaji mkono wa sera za EU |
Matokeo hayo yameonekana uidhinishaji wa sera za waziri mkuu Aleksandar Vuchich za kuunga mkono Umoja wa Ulaya (EU).
5. Sisi asihi raia Misri wakatae maandamano
![]() |
Makundi yanayopinga utawala wa Al-Sisi yamepanga maandamano leo |
Bw Sisi anasema kuwa jitihada za kuyumbisha amani nchini Misri, hazitafua dafu, ikiwa tu raia wa taifa hilo watasimama kidete.
Uhasama dhidi ya serikali umeongezeka majuzi baada ya utawala wa nchi hiyo kuipa Saudi Arabia visiwa viwili vilivyoko katika eneo la Bahari ya Sham.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten