RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE.
Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda ameiambia
Nipashe katika mahojiano maalumu katikati ya wiki kuwa Kikwete
ameshawasilisha tamko la mali zake tangu aondoke madarakani Novemba 5,
mwaka jana.
Jaji Kaganda alisema Kikwete aliwasilisha fomu inayoonyesha mali
alizozipata wakati akiwa madarakani kati ya 2005-2015, na alizozipata
kabla hajangia madarakani kwa Sekretarieti yake.
Nipashe ilizungumza na Jaji Kaganda kujua kama Kikwete alishatoa tamko
kama Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 na
kanuni zake zinavyoelekeza, lakini pia kufahamu idadi ya mali
anazomiliki Rais huyo mstaafu na thamani yake.
Kaganda alisema ni kweli Kikwete aliorodhesha mali zake zote kwa tume
lakini Jaji huyo alikataa katakata kumwonyesha mwandishi wa habari hizi
tamko hilo.
Jaji Kaganda alisema sheria inazuia kumwonyesha mtu mwingine tamko la
mali la mtu mwingine hadi kuwe na sababu ya maana ya anayehitaji, na pia
kuwe na ulazima wa kufanya hivyo.
"Mwananchi anaweza kupata taarifa za mali za viongozi kwa kufuata
utaratibu uliopo, lakini baada ya kupata taarifa hizo, haruhusiwi
kuzitangaza au kuzichapisha kwenye vyombo vya habari,” alisema Jaji
Kaganda.
Kwa mujibu wa kifungu kifunga 9(1) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma, “Kila kiongozi wa umma atatakiwa katika kipindi cha miezi mitatu
au katika kipindi cha siku thelathini baada ya kupata wadhifa, mwisho wa
mwaka au mwisho wa kutumikia wadhifa wake kumpelekea Kamishna tamko la
maandishi katika hati rasmi linaloorodhesha mali au rasilimali zake.”
Aidha, kifungu namba 9 (6) kinataka “Wakati wa kutoa tamko la rasilimali
zake kwa mujibu wa fungu hili, kiongozi wa umma atatakiwa: (a) kutaja
thamani ya mali aliyotamka na chanzo au namna alivyopata mali hiyo."
Kifungu namba 11 (2) cha sheria hiyo kinaeleza kuwa rasilimali
zinazotakiwa kutajwa ni pamoja na (a) nyumba, mali ya starehe na
mashamba yanayotumiwa au yanayotarajiwa kutumiwa na viongozi wa umma au
familia zao.
Kifungu 2 (b) kinataka kutajwa kwa kazi za sanaa, mambo ya kale na vitu
alivyonunua kidogokidogo; (c) magari na aina nyingine binafsi za usafiri
kwa matumizi binafsi; (d) fedha taslimu na amana zilizowekwa benki au
taasisi nyingine za fedha.
Kifungu 2 (e) kinataka taarifa za hawala za hazina na uwekezaji mwingine
katika dhamana zenye thamani maalumu, zinazotolewa au kudhaminiwa na
serikali au wakala wa serikali.
SH. MILIONI 25
Wakati viongozi wengi wa umma wakitaja mali zao kwa Tume ya Maadili tu
ama kushindwa kutaja mali hizo huko kwa mujibu wa sheria, Waziri Mkuu
mstaafu, Mizengo Pinda ana historia ya peke yake.
Pinda alitaja mali anazomiliki ambazo miongoni mwake ni nyumba mbili
pamoja na akaunti katika benki, zilizokuwa na fedha zisizozidi Sh.
milioni 25 Januari 15, 2010.
Pinda alisema alikuwa akimiliki nyumba moja mjini Dodoma na nyingine Mpanda, mkoani Rukwa eneo la Makanyagio.
Aidha alisema alikuwa na kibanda shambani kwake Pugu, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
“Mimi kila mwaka nataja mali zangu kwa Tume (Sekretariati ya Maadili ya
Viongozi wa Umma)," alisema Pinda wakati huo akiwa madarakani.
"Sijaulizwa, sijagombana na Tume.
"Ukiniuliza ni masikini kiasi gani, nitakwambia nina property (nyumba)
Dodoma, nimejenga kwa utaratibu wa serikali wa kuomba mkopo, ninayo
nyingine kwetu Mpanda pale Makanyagio.
“Dar es Salaam sina nyumba, pale Pugu nina nyumba kidogo, inahitaji kazi ya ziada.
"Kijijini nilikuwa nafikia kwa babu, babu ana kanyumba kake ka ovyo
ovyo… kile ambacho mlikiona, ana vyumba viwili nilikuwa nalala pale,
lakini baada ya Uwaziri Mkuu, jamaa wakaniambia aah… haiwezekani pale.
"Nilijua nitaweza kulala pale na hawa jamaa (wasaidizi wake) watalala mjini humo, nikaambiwa hapafai.”
Pinda ambaye wakati huo alikuwa pia Mbunge wa Mpanda Mashariki, alisema
hana gari lolote zaidi ya alilopewa kwa kuwa Mbunge, na kwamba katika
akaunti zake zote, wakati huo alikuwa na Sh. milioni 22 hadi 25 tu.
Abonneren op:
Reacties posten (Atom)
ALIKIBA NCHINI UJERUMAN
Follow us on facebook
Popular Posts
-
Leo tutaongelea kuhusu furaha na afya katika michezo mbalimbali ndani ya jamii. Kuna aina za michezo nyingi sana katika jamii hivyo basi ...
-
Miongozo mipya iliyotolewa nchini Marekani inapendekeza wanawake wajawazito kufanya mazoezi mepesi karibu siku zote za ujauzito. Tofauti...
-
Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimbo la "putter" Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimb...
-
MUONEKANO WA HALISI WA BAO NA KETE ZAKE Habari ndugu msomaji wa makala hii ya Ielewe Michezo leo tutakuwa tukiangazia juu ya m...
-
Lionel Messi Lionel Andrés Messi (amezaliwa Rosario, Argentina , 24 Juni 1987 ) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka ...
-
hiki ni kibao cha chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha <AJTC> hili ni jengo la utawala katika chuo cha uan...
-
Syria imetangaza usitishaji wa mapigano wa muda mfupi karibu na Damascus na katika jimbo moja lakini haikutaja juu ya mapigano katika me...
-
1. Ni sayari ambayo kila baada ya miaka 3600 huingia katika solar system yetu na huikaribia dunia ila haitaigonga dunia. 2. Ni sayari am...
-
Nchi inaweza kuwa maskini zaidi duniani kama wana Pato duni la Asili , Kuna rasilimali kidogo, ukosefu wa ajira na maendeleo ...
-
Aliyekuwa mke wa rapa Wiz Khalifa ‘Amber Rose’ amejitamba hivi karibu akiwa na mp...
Geen opmerkingen:
Een reactie posten