Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka
12, Qasama Machibya aliyejifanya ofisa usalama wa Taifa kwenye ziara ya
Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2013.
Kabla ya hukumu, mshtakiwa alijitetea mahakamani hapo kuwa kitambulisho
alichokutwa nacho siyo chake na anashangaa kuona kuna picha yake na jina
lake.
Alidai kuwa hizo ni mbinu za polisi kumminya, hivyo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba ana ugonjwa wa Ukimwi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila alisema
utetezi wa mshtakiwa hauifanyi mahakama kutomtia hatiani kwa kuwa hana
cheti cha ugonjwa.
Alisema kutokana na mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilishwa inamtia hatiani kwa makosa matatu.
Kurwijila alisema kosa la kwanza ni kughushi nyaraka ya Serikali hivyo,
atakwenda jela miaka mitano na kosa la pili la kujifanya ofisa usalama
wa Taifa kifungo chake ni miaka miwili.
Alisema katika kosa la tatu la kuudanganya umma kwa kutoa nyaraka iliyoghushiwa hivyo, atatumikia adhabu gerezani miaka mitano.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elias Mgobela alisema mshtakiwa alikamatwa
wakati Kikwete alipokuwa akitarajia kuhutubia wananchi kwenye mkutano
wa hadhara.
Abonneren op:
Reacties posten (Atom)
ALIKIBA NCHINI UJERUMAN
Follow us on facebook
Popular Posts
-
Leo tutaongelea kuhusu furaha na afya katika michezo mbalimbali ndani ya jamii. Kuna aina za michezo nyingi sana katika jamii hivyo basi ...
-
Miongozo mipya iliyotolewa nchini Marekani inapendekeza wanawake wajawazito kufanya mazoezi mepesi karibu siku zote za ujauzito. Tofauti...
-
Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimbo la "putter" Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimb...
-
MUONEKANO WA HALISI WA BAO NA KETE ZAKE Habari ndugu msomaji wa makala hii ya Ielewe Michezo leo tutakuwa tukiangazia juu ya m...
-
Lionel Messi Lionel Andrés Messi (amezaliwa Rosario, Argentina , 24 Juni 1987 ) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka ...
-
hiki ni kibao cha chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha <AJTC> hili ni jengo la utawala katika chuo cha uan...
-
Syria imetangaza usitishaji wa mapigano wa muda mfupi karibu na Damascus na katika jimbo moja lakini haikutaja juu ya mapigano katika me...
-
1. Ni sayari ambayo kila baada ya miaka 3600 huingia katika solar system yetu na huikaribia dunia ila haitaigonga dunia. 2. Ni sayari am...
-
Nchi inaweza kuwa maskini zaidi duniani kama wana Pato duni la Asili , Kuna rasilimali kidogo, ukosefu wa ajira na maendeleo ...
-
Aliyekuwa mke wa rapa Wiz Khalifa ‘Amber Rose’ amejitamba hivi karibu akiwa na mp...
Geen opmerkingen:
Een reactie posten