Kitengo cha usalama nchini Sudan
kimewaachiliwa huru wanafunzi sita wanaofanya uanaharakati waliokuwa
wakizuiliwa bila mashtaka tangu msururu wa maandamano katika mji mkuu
mnamo mwezi Mei, wakili wao amesema.
Wanafunzi sita ambao ni wanaharakati wa kijamii wameachiliwa huru lakini wengine wanane wangali wanazuiliwa na idara ya ujasusi nchini Sudan NISS.
Vyanzo vya kibalozi ambavyo viko karibu na familia ya wanafunzi hao vimethibitisha kuwa wanafunzi hao wameachiliwa na vimesema kuwa wale walioko kizuizini huenda wakafunguliwa mashtaka.
Wakili wa wanafunzi hao amesema kuwa mazungumzo yanaendelea ili kujaribu kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanarejelea masomu yao katika chuo kikuu baada ya kutimuliwa na wasimamizi kufuatia maandamano hayo.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadam yameelezea wasi wasi kuhusiana na usalama wa wanafunzi hao ambao wako kizuizini.
Shirika la kimataifa la haki za kibinadam International Federation of Human Rights (FIDH) limesema kuwa limenakili visa kadhaa vya wanafunzi hao kudhulumiwa pamoja na wafungwa wengine.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten