burudan

Misaada zaidi yahitajika Syria

Ndege za kugawa misaada Syria
Marekani ,Ufaransa na Uingereza wametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuanza kutoa misaada ya kibinadamu kwa maeneo yaliyoathirika nchini Syria.

Wamesema serikali ya Rais Assad imeshindwa kuheshimu muda wa mwisho, ambao ni mwezi Juni mwaka huu, kwa ajili ya usambazaji wa vifaa vya lazima kwa wahitaji
.
Siku ya Jumatano msafara wa kutoa misaada ulifikia katika mji wa Daraya,ambao umezingira na vikosi vya serikali kwa takribani miaka minne hadi sasa,lakini haukuwa na vyakula
.
Urusi imesema kuwasili kwa msafara huo ni hatua muhimu sana. Waziri wa masuala ya kigeni wa Uingereza amesema kukwama kwa misaada hiyo kunasababishwa na Assad mwenyewe.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa litakutana Ijumaa ijayo ili kujadili utoaji misaada nchini humo.

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates