Mbunge
wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alikuwa mkali
bungeni akisema yeye si mwizi na kuwabeza wanaomuita hivyo kuwa
wataisoma namba.
Profesa Tibaijuka alifikia hatua hiyo baada ya kuhamaki kutokana na
baadhi ya wabunge wa upinzani kupaza sauti na kumuita mwizi wakati
akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Profesa Tibaijuka alianza kwa kuwataka wabunge wamuunge mkono Rais John Magufuli kwa kuwa amechaguliwa na wananchi.
“Wenzetu ambao kazi yao ni kuja kutusimamia sisi (upinzani) wana haki ya
kusema wanayoyasema, lakini hata sisi tuna haki ya kuyaweka vizuri ili
yaeleweke kwa wananchi,” alisema.
Profesa Tibaijuka alisema upinzani ukifilisika utabaki kukemea kwa
sababu ni lazima tu useme kitu, Bunge linageuka kijiwe na bungeni si
mahali pa kupeleka hoja za vijiweni.
Kauli hiyo iliwakera wabunge wa upinzani ambao walianza kupaza sauti zao dhidi yake, hali iliyoonekana kumchanganya.
Akirejea hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu
kuwa Tanganyika inainyonya Zanzibar na kuifanya koloni lake, Profesa
Tibaijuka alihoji: “Tanganyika inainyonya Zanzibar katika lipi? Hili ni
jambo la kujiuliza. Nimejiuliza mimi kama mchumi. Kazi yangu ya kwanza
nyinyi mnanijua nilikuwa kwenye shirika la makazi duniani, hamjui kwamba
nilikuwa kwenye Shirika la Biashara la Dunia?” alihoji.
Kutokana na zomeazomea kuendelea, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliingilia
kati: “Waheshimiwa wabunge namlinda mzungumzaji, naomba muwe wavumilivu.
Mheshimiwa Profesa endelea."
“Kwa wale wanaosema nimeiba mtaisoma namba, mimi si mtu wa kutishwa na vitu vya ovyoovyo.
"Mimi sitishwi na hoja za ovyoovyo, huyo (mtu) akaisome namba. Nasimama
hapa kwa sababu nataka nitetee vitu. Mtu anapopotosha anaweza kuleta
hatari. Tanganyika kwa mtizamo wa kiuchumi haiwezi kuinyonya Zanzibar.
“Katika Dunia ya ustaarabu unasikia hoja. Lissu hapa angeweza kuzomewa,
lakini wastaarabu wakamsikiliza wamekomaa kisiasa,” alisema huku baadhi
ya wabunge wakiendelea kumzomea.
Tibaijuka aliwahi kuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete na aliondolewa baada ya
kutuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow
Abonneren op:
Reacties posten (Atom)
ALIKIBA NCHINI UJERUMAN
Follow us on facebook
Popular Posts
-
Leo tutaongelea kuhusu furaha na afya katika michezo mbalimbali ndani ya jamii. Kuna aina za michezo nyingi sana katika jamii hivyo basi ...
-
Miongozo mipya iliyotolewa nchini Marekani inapendekeza wanawake wajawazito kufanya mazoezi mepesi karibu siku zote za ujauzito. Tofauti...
-
Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimbo la "putter" Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimb...
-
MUONEKANO WA HALISI WA BAO NA KETE ZAKE Habari ndugu msomaji wa makala hii ya Ielewe Michezo leo tutakuwa tukiangazia juu ya m...
-
Lionel Messi Lionel Andrés Messi (amezaliwa Rosario, Argentina , 24 Juni 1987 ) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka ...
-
hiki ni kibao cha chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha <AJTC> hili ni jengo la utawala katika chuo cha uan...
-
Syria imetangaza usitishaji wa mapigano wa muda mfupi karibu na Damascus na katika jimbo moja lakini haikutaja juu ya mapigano katika me...
-
Nchi inaweza kuwa maskini zaidi duniani kama wana Pato duni la Asili , Kuna rasilimali kidogo, ukosefu wa ajira na maendeleo ...
-
1. Ni sayari ambayo kila baada ya miaka 3600 huingia katika solar system yetu na huikaribia dunia ila haitaigonga dunia. 2. Ni sayari am...
-
Huu ni mji wa Monaco ukitaka kununua luxury property gharama yake ni $ 1 million kwa 16 square meters Monaco hiyo. Yani ukubwa wa uwanja...
Geen opmerkingen:
Een reactie posten