burudan

Ujumbe wa kuwepo moshi ndani ya ndege ulipokelewa


Ndege ya EgyptAir ilikuwa na watu 66.
Wachunguzi nchini Ufaransa wamethibitisha ripoti kuwa ndege ya EgyptAir ilituma ujumbe kuwa moshi ulikuwa kwenye ndege hiyo muda mfupi kabla ianguke katika bahari ya Mediterrania.
Shirika la usalama wa safari za ndege linasema kuwa ujumbe huo unamaanisha kuanza kwa moto.

Ujumbe huo ulipokelewa muda mfupi kabla ya ndege hiyo aina ya Airbus A320 kutoweka kutoka kwa mitambo ya radar siku ya Alhamisi.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka mjini Paris, Ufaransa na jumla ya watu 66.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya Usalama anasema kuwa ajali hiyo huenda ikawa ni ya kawaida au ilisababishwa na mlipuko . Hata hivyo alisema uhakiki hauwezi kujulikana kwa sasa hadi chombo maalumu cha kunasa mawasiliano kwenye ndege kitakapopatikana na kuchunguzwa

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates