![]() |
Semenya anatarajiwa kushinda dhahabu Olimpiki |
Mwanariadha Caster Semenya kutoka
Afrika Kusini ameshinda mbio za 800m za wanawake katika mashindano ya
Diamond League yaliyofanyika Rabat, Morocco.
Semenya, 25, alifanyiwa uchunguzi wa kubaini jinsia yake kamili baada yake kushinda dhahabu mashindano ya ubingwa wa riadha ya mwaka 2009.
Anapigiwa upatu kushinda dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu mjini Rio 2016, ambapo anapanga pia kukimbia mbio za 400m.
Mwingereza Lynsey Sharp alimaliza wa tano.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten