Mshambuliaji wa klabu ya Manchester
United na Uingereza Wayne Rooney amesema kuwa huenda akaanza kucheza
katika safu ya kati katika siku za usoni baada kucheza vyema katika safu
hiyo dhidi ya Bournemouth katika uwanja wa Old Trafford.
Nahodha huyo wa kikosi cha Uingereza alifunga bao la kwanza kabla ya kumpatia pasi nzuri Ashley young kwa bao la tatu.
''Mara nyengine unafaa kuamua katika kazi yako na kwa sasa ni bora mimi kucheza katika safu ya kati'',alisema.
''Inaweza kuwa tofauti kwa timu ya Uingereza ambapo ninaweza kuwa mshambuliaji, lakini pengine msimu ujao huenda nikacheza katika safu hiyo''
Geen opmerkingen:
Een reactie posten