Hutakiwi kushangaa siku ukisikia lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond
kuwa ipo juu zaidi ya Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy, hiyo ni
kutokada na mikakati pamoja na jitihada zinazozidi kuwekwa na uongozi
wa lebo hiyo.
Mpaka sasa lebo ya WCB inawamiliki wasanii wanne akiwemo Diamond,
Harmonize, Raymond na Q Boy Msafi huku kukiwa na taarifa za chini chini
kuwa tayari Rich Mavoko ameshamwaga wino wa kuwa chini ya lebo hiyo huku
bajeti yake ikiwa tayari imeshawekwa pembeni na tayari amesharekodi
wimbo pamoja na video iliyofanyika huko Afrika Kusini. Lakini pia nje ya
kutafuta vipaji kwenye hili analolifanya Diamond ni biashara kubwa
ambayo itafanya akaunti zake za benki kujaa kila siku.
Hiki ndicho kitaweza kuipaisha lebo ya WCB kuwa kubwa zaidi.
Ukubwa wa jina la Diamond
Hili halina ubishi kwa sasa Diamond amekuwa ni miongoni mwa wasanii
wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki kwa Afrika kwa sasa. Hicho
ni kitu ambacho kimemfanya kujitengenezea fan base kubwa kutokana na
kazi zake anazofanya, lakini pia ana uwezo wa kuwatengenezea connection
wasanii wa lebo yake [WCB] kufanya kazi na msanii yeyote wa Afrika
endapo muda utaruhusu kutokana na jina lake huku yeye mwenyewe akizidi
kujitafutia connection za Marekani na Ulaya kama walivyoanza kwa
Harmonize kufanya kazi na Korede Bello kutoka Mavin Records lakini pia
Harmonize aliwahi kusema ana kazi na Kiss Daniel wa Nigeria.
Mashabiki wanaomsupport Diamond
Diamond ni msanii mwenye washabiki wengi wanaomsupport ambao wapo
tayari kupambana na lolote endapo wataona msanii wao anaandamwa na na
maneno kutoka upande mwingine. Kutokana na hilo uongozi wa WCB unaweza
kutumia pointi hiyo kuifanya lebo yao kuwa juu zaidi kama wanavyofanya
sasa kwa Harmonize na Raymond kutembelea nyota ya Dangote.
Menejimenti ya WCB
Uongozi wa WCB ukiongozwa na Salaam pamoja na Babu Tale umefanikiwa
kufaulu kwenye suala la mipango na kujiamini kwenye kila wanalolifanya
na hawashindwi kujaribu. Kutokana na uwezo wao walionao wanaweza
wakaifanya lebo ya WCB kufika mbali zaidi lakini itachukua muda mpaka
kufika huko.
Abonneren op:
Reacties posten (Atom)
ALIKIBA NCHINI UJERUMAN
Follow us on facebook
Popular Posts
-
Leo tutaongelea kuhusu furaha na afya katika michezo mbalimbali ndani ya jamii. Kuna aina za michezo nyingi sana katika jamii hivyo basi ...
-
Miongozo mipya iliyotolewa nchini Marekani inapendekeza wanawake wajawazito kufanya mazoezi mepesi karibu siku zote za ujauzito. Tofauti...
-
Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimbo la "putter" Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimb...
-
MUONEKANO WA HALISI WA BAO NA KETE ZAKE Habari ndugu msomaji wa makala hii ya Ielewe Michezo leo tutakuwa tukiangazia juu ya m...
-
Lionel Messi Lionel Andrés Messi (amezaliwa Rosario, Argentina , 24 Juni 1987 ) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka ...
-
hiki ni kibao cha chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha <AJTC> hili ni jengo la utawala katika chuo cha uan...
-
Syria imetangaza usitishaji wa mapigano wa muda mfupi karibu na Damascus na katika jimbo moja lakini haikutaja juu ya mapigano katika me...
-
1. Ni sayari ambayo kila baada ya miaka 3600 huingia katika solar system yetu na huikaribia dunia ila haitaigonga dunia. 2. Ni sayari am...
-
Nchi inaweza kuwa maskini zaidi duniani kama wana Pato duni la Asili , Kuna rasilimali kidogo, ukosefu wa ajira na maendeleo ...
-
Aliyekuwa mke wa rapa Wiz Khalifa ‘Amber Rose’ amejitamba hivi karibu akiwa na mp...
Geen opmerkingen:
Een reactie posten