burudan

Amber Rose apanga kumualika Wiz Khalifa kwenye kipindi chake cha TV

Mwanamitindo maarufu asiyeishiwa vituko, Amber Rose amepanga kumualika Wiz Khalifa kwenye show yake ya ‘Amber Talk Show’.
Amber-Rose-files-for-divorce-from-Wiz-Khalifa
Siku chache zilizopita Amber Rose alidai kuwa atakuwa na furaha kubwa kumkaribisha mume wake wa zamani katika kipindi hicho kwa ajili ya kuelezea maisha yake.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wiz Khalifa alisema ataenda kupita tu, hatokuwa na muda wa kupoteza, lakini anashukuru sana kwa kupewa nafasi hiyo kuwa mgeni rasmi kwenye show hiyo.
Aidha wawili hao walifanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume, Sebastian (3) lakini mahusiano yao yalivunjika mwaka jana.

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates