Straika
wa Leicester City, Jamie Vardy anatarajiwa kuikosa mechi dhidi ya
Manchester United kutokana na kukubali kupokea adhabu baada ya kupewa
kadi nyekundu kwa kumbugudhi mwamuzi wakati wa mechi dhidi ya West Ham
United.
Chama
cha Soka cha England (FA) kilisema kitamwongeza adhabu mchezaji huyo
kwa tukio lake hilo la kumsumbua mwamuzi Jon Moss baada ya kupewa kadi
nyekundu kwa kujirusha ndani ya eneo la 18 la West Ham, lakini FA ilitoa
muda mpaka jana jioni kuwa anaweza kukata rufaa.
Taarifa iliyotolewa jana jioni ilieleza kuwa Vardy amekubali kosa na yupo tayari kwa adhabu.
Ikiwa
atapewa adhabu anaweza kuikosa mechi dhidi ya Swansea City, wikiendi
hii pamoja na ile inayofuata dhidi ya Manchester United mnamo Mei 1,
2016.
Kukosekana kwa straika huyo kunaweza kuathiri katika mbio
za ubingwa wa Premier League kwa timu yake inayoshika usukani wa ligi
ikiwa pointi tano mbele ya Tottenham.
MECHI ZA LEICESTER CITY ZILIZOSALIA
April 24 Swansea City (nyumbani)
May 1 Manchester United (ugenini)
May 7 Everton (nyumbani)
May 15 Chelsea (ugenini)
MECHI ZA TOTTENHAM ZILIZOSALIA
April 25 West Bromwich Albion (nyumbani)
May 2 Chelsea (ugenini)
May 8 Southampton (nyumbani)
May 15 Newcastle United (ugenini)
Abonneren op:
Reacties posten (Atom)
ALIKIBA NCHINI UJERUMAN
Follow us on facebook
Popular Posts
-
Leo tutaongelea kuhusu furaha na afya katika michezo mbalimbali ndani ya jamii. Kuna aina za michezo nyingi sana katika jamii hivyo basi ...
-
Miongozo mipya iliyotolewa nchini Marekani inapendekeza wanawake wajawazito kufanya mazoezi mepesi karibu siku zote za ujauzito. Tofauti...
-
MUONEKANO WA HALISI WA BAO NA KETE ZAKE Habari ndugu msomaji wa makala hii ya Ielewe Michezo leo tutakuwa tukiangazia juu ya m...
-
Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimbo la "putter" Mchezaji akicheza mpira karibu na shimoni kwa fimb...
-
1. Ni sayari ambayo kila baada ya miaka 3600 huingia katika solar system yetu na huikaribia dunia ila haitaigonga dunia. 2. Ni sayari am...
-
Lionel Messi Lionel Andrés Messi (amezaliwa Rosario, Argentina , 24 Juni 1987 ) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka ...
-
Nchi inaweza kuwa maskini zaidi duniani kama wana Pato duni la Asili , Kuna rasilimali kidogo, ukosefu wa ajira na maendeleo ...
-
Even John Cena was hypnotized by his GF Nikki Bella’s cleavage during an event in NYC. The WWE Diva — with a huge hand from her l...
-
Waziri wa michezo Fikile Mbalula Afrika Kusini haitaandaa mashindano ya Raga, Kriketi, Riadha na Netiboli baada ya se...
-
Poda ya Johnson, iliyodhaniwa kuwa ni kipodozi na tiba mujarabu kwa watoto na watu wazima duniani kote imebainika kusababisha saratani. ...






Geen opmerkingen:
Een reactie posten