![]() |
kuunganisha taifa |
Kamati ya pamoja inayosimamia mpango
wa Amani nchini Sudan Kusini imeitisha mkutano wa dharura kujadili
switafahamu inayokumba kurejea kwa kiongozi wa waasi Riek Machar jijini
Juba.
Nayo wizara ya maswali ya kigeni ya Marekani pia imeeleza kusikitika kwake na Machar, huku ikidai Machar anachelea kufika Sudan kimakusudi.
Aidha kamati ya kusimamia mkataba wa Amani nchini humo pia imeeleza masikitiko yake dhidi ya Machar, lakini vilevile ikaipa changamoto serikali ya Sudan Kusini kulegeza kamba ili kumwezesha Machar kurejea.
Lakini serikali ilijibu kuwa Machar alitaka kuingia nchini na idadi isiyokubalika ya wanajeshi na silaha nzito.
Msemaji wa Machar Mabior Garang alisema serikali inadanganya, na kuashiria kuwa Riek Machar atawasili Juba hii leo kusipokuwa na hitilafu.
Kurejea kwa Machar ni hatua muhimu ya kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa sahihi mwezi Agosti mwaka jana.
Iwapo atarejea, ataapishwa kama makamu wa rais , kisha kutakiwa kuunda serikali ya muungano na rais Salva Kiir.
Tangu hapo maelfu ya watu wameuawa, huku zaidi ya watu milioni mbili wakipoteza makao.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten