![]() |
Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda
wahamiaji wapatao 700 wanahofiwa kufariki katika kipindi cha siku tatau
zilizopita katika bahari ya Mediterranean.
Wahamiaji waliokololewa juma lililopita kutoka katika boti moja kwenye bahari ya Mediterranea, wamewaambia wafanyikazi wa makundi ya uokoaji kuwa, waliona chombo kimoja cha baharini kilichojaa wakimbizi kikizama
.
Shirika moja la uokoaji la Save the Children, limeiambia BBC kuwa manusura hao walisema kuwa walingoa nanga katika msafara wa maboti matatu Jumatano usiku kutokea Libya.
Maafisa wa Polisi wa Italia wanasema waliwahoji wahamiaji hao waliofika mjini Sicily hapo Jana Jumamosi.
Juma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten