burudan

Watanzania waadhimisha Siku ya Muungano bila sherehe



Magufuli
Image captionMagufuli aliagiza pesa za sherehe zitumiwe kukarabati barabara Mwanza
Watanzania wameadhimisha Siku ya Muungano bila sherehe, baadhi wakiamua kutumia sikukuu hiyo kufanya usafi.
Rais wa Tanzania John Magufuli aliahirisha sherehe na badala yake akawataka Watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani au wakiwa katika shughuli zao binafsi.
Siku hiyo hata hivyo bado ilisalia kuwa ya mapumziko kama kawaida.
Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alitembelea Uwanja wa Taifa unaotumika ambao kawaida hutumika katika sherehe za taifa.
Uwanja huo umefungwa na hakuna shamrashamra zozote zinazoendelea.
Katika eneo la Temeke, karibu na uwanja huo wa taifa, aliwakuta vijana wakifanya usafi.
Temeke
Image captionVijana katika eneo la Temeke wamekuwa wakifanya usafi
Siku ya Muungano huadhimishwa tarehe 26 Aprili kila mwaka kukumbuka siku sawa na hiyo mwaka 1964 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja).
Dkt Magufuli alisema fedha ambazo zilipangwa kutumika kwa ajili ya kugharimia vinywaji, vyakula, gwaride, halaiki, burudani mbalimbali na hafla ya usiku zitumike kupanua barabara ya Mwanza Airport katika eneo linaloanzia Ghana Quarters hadi uwanja wa ndege wa Mwanza.
Sherehe
Image captionSherehe zingegharimu karibu bilioni mbili za Tanzania
Inakadiriwa kwamba sherehe zingegharimu takriban shilingi bilioni mbili za Tanzania sawa na dola milioni moja za Kimarekani.
Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi kutatua msongamano wa mkubwa wa magari ambayo umekuwa ukiathiri shughuli eneo hilo.
<

Geen opmerkingen:

Een reactie posten

KBSBLOG Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Thema-afbeeldingen van Bim. Mogelijk gemaakt door Blogger.
Published By Gooyaabi Templates