Polisi nchini India wanasema kuwa
zaidi ya watu 100 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa katika moto
uliotokea katika hekalu la Wahindu katika jimbo la Kusini la Kerala.
Polisi wanasema huenda moto huo ulianzishwa na fataki.
Waziri wa mashauri ya nchini katika jimbo la Kerala, Ramesh Chentallah, alisema kuwa uchunguzi wa mahakama utaanzishwa
Waziri wa Mashauri ya Ndani, Oommen Chandi, na bwana Ramesh wamesema kuwa watatembelea eneo hilo.
Polisi wamesema kuwa moto huo umedhibitiwa lakini shughuli za uokozi zingali zinaendelea.
Maelfu ya waumini walikuwa wamekongamana ilikushuhudia maonesha haya ya kila mwaka ya fata
Uchunguzi wa kwanza umebaini kuwa maafisa wakuu katika eneo hilo waliwanyima waratibu wa maonesho hayo leseni ya kuandaa maonesho ya fataki kufuatia hofu kuhusu usalama wa umma.
Waziri mkuu wa India bwana Narendra Modi amewasili Kerala.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten