![]() |
Miongoni mwa vurugu zilizotokea mji mkuu wa Bujumbura |
Waziri wa zamani wa Rwanda Jacques
Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada
ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni "mauaji".
Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten