Rais wa Ufaransa Francois Hollande
amesema habari zilizopatikana kufikia sasa zinaashiria ndege ya shirika
la ndege la EgyptAir iliyotoweka ikiwa safarini kutoka Paris kwenda
Cairo ilianguka.
"Taarifa tulizokusanya kufikia sasa, mawaziri, maafisa wa serikali na, bila shaka, maafisa wa Misri, zinathibitisha, kwa huzuni, kwamba ndege ilianguka. Ilitokomea.”
Bw Hollande ameahidi kwamba serikali yake itatoa usaidizi unaohitajika na maafisa wa Ugiriki na Misri wanaoendelea na juhudi za kuisaka ndege hiyo.
Ndege hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia mmoja mmoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria, Sudan, Chad na Ureno.
Waziri Mkuu wa Misri Sherif Ismail ameambia wanahabari kwamba juhudi za kuitafuta ndege hiyo bado zinaendelea.
Maafisa wa Misri na Ugiriki wanatumia ndege na meli kuitafuta ndege hiyo katika bahari ya Mediterranean.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba watu 66 ilipotoweka kilomita 16 ndani ya anga ya Misri.
Geen opmerkingen:
Een reactie posten